E-learning - Dar es Salaam, Dar es Salam, Tanzania
Sisi ni timu ya watu wanaomini msemo wa "Elimu haikuanzia darasani, mama alianza kufundisha. Elimu haishii darasani, mtaa unaendelea kufundisha."- Rogers Katuma Watu wengi wamekosa fursa ya kuendelea kielimu kupitia mfumo wa kawaida wa elimu, kwenda shule, kufaulu na kupata cheti. Na watu wengi zaidi wanakosa fursa ya kujiendeleza kielimu baada ya sehemu waliyoishia shuleni kutokana na gharama, majukumu, muda na mfumo. Kiuhalisia mtaani kuna elimu, ujuzi na uwezo tofauti unaohitajika ili ufanikiwe hata kama hamna anayetoa cheti. Njia bora zaidi ya kujifunza ni kupitia ujuzi, elimu na uzoefu ambao umefanya kazi mtaani na kufikisha malengo ya watu. Na watu bora zaidi wa kufundisha ni wale ambao ujuzi, elimu na uzoefu wao mtaani umewafanya wafanikiwe. Sisi ni timu ya watu tunaotengeneza mazingira ya watu wenye ujuzi, elimu na uzoefu waliofanikiwa mtaani na kuifikisha kwa watu walioukuwa darasani na waliotoka darasani wakiwa kwenye safari yao ya mafanikio mtaani. Ndoto yetu ni kuhakikisha kila mwenye macho, masikio na simu apate ujuzi, elimu na uzoefu inayohitajika kufanikiwa mtaani. "Elimu haikuanzia darasani, mama alianza kufundisha. Elimu haishii darasani, mtaa unaendelea kufundisha."- Rogers Katuma
Nginx
Google Tag Manager
Google Font API
Google Analytics
Vimeo
Mobile Friendly